Msimamizi wa mchezaji wa Yanga SC Jasmin, Razack amedai Clement Mzize ambaye ni mteja wake hawezi kuuzwa kama ng' ombe mnadani isipokuwa wanatakiwa kumpa nafasi aamue.
"Mchezaji hauzwi uzwi tu kama Ng'ombe mnadani Kuna sheria na taratibu zake, Umesema Kuna Klabu Yanga wamekubali ofa lakini Mzize hajakubali kikubwa ni kufuata sheria na kanuni, Kama Klabu kwa Klabu wamekubaliana inabaki upande wa Mchezaji kwenye "Personal Terms" ila Hawezi kuuzwa tu kama Ng'ombe Mnadani", Mchezaji sio mtumwa ni ajira kama ulivyoajiriwa Wewe hapo.
.
"Sisi Mpaka sasa ofa rasmi tuliyoipokea kwaajili ya Mchezaji huyo ni ofa kutoka Al masry ambayo mwisho wake ni Leo , Al Masry tuliongea na Sports Director wao pamoja na president wa Klabu lakini Bado hatujapata majibu kutoka Yanga"
.
"Mzize Bado anamkataba na Yanga aliongeza mwakajana tu mkataba wa miaka mitatu kwahiyo Bado anamkataba wa miaka mitatu na Yanga"
.
"Hizo ofa nyingine unazosema sijui Yanga amekubali ofa ya Wapi sijui ya wapi sisi hatuna/ hatujapata ofa hizo na sisi hatuwezi kujibu Maneno, tunajibu ofa za maandishi na kama ambavyo nimekuambia ofa ya maandishi ambayo tulikuwa nayo ni ya Al masry ambayo mwisho wake ulikuwa ni Leo" - Yasmini Razack akihojiwa na EFM juu ya Clement Mzize.