Mzamiru Yassin alikuja Simba 16/17, mwaka 2022 akaongeza mkataba wa miaka miwili hadi 2024, akaongeza tena miwili hadi 2026, msimu huu ukiisha Mzamiru anakuwa Free Agent.
-
Katika muda wote akiwa Simba SC, Mzamiru hajawahi kuwa mbaya bonge moja la Mido, ila lazima tukubali muda wake umeisha na hakuna kipya ataprove Simba, kuzingatia na umri, pia alishatumika.
-
Simba iliyocheza robo fainali mara nne, ubingwa wa ligi mfululizo huyu kiumbe alikuwepo tena alicheza kwa juhudi sana, kuna wakati lazima tukubali kila nabii na zama zake.
-
Zama za Mzamiru zinaelekea ukingoni, majeraha pia yamechangia, ila kwa umri wake 33+ na majeruhi aliyokuwa nayo, tukubali Mzamiru kazi imeisha, hakuna miujiza mipya kwake tena.
-
Kabakisha mwaka mmoja, wasiwasi ni kuwa hata anaweza asipate game time msimu huu, na msimu ujao akiwa free ukamkuta Namungo huko.
-
Kwa umri wa Mzamiru na mahitaji ya Fadlu, utamuanzisha Mzamiru, Kante? au Kagoma? wakae nje hapana.
-
Simba iliyopoteza ubingwa misimu minne haiwezi kuendelea kumtegemea au kuamini kuwa Mzamiru atakuja kuwa regular au mchezaji wakutegemewa tena. Hana msimu mmoja na nusu kuanzia sasa.