Ningekuwa Mkude au John Bocco nisingependa siku ya tukio la kuagwa na Simba kwa sababu Simba wana mtindo wa kuchafua taswira za Malegend wao kwa makusudi kabisa
Ameondoka Aishi Manula hawajampa heshima yoyote kabisa na hajaenda Yanga ameenda Azam kwanini sahivi Aishi hapewi Ile thamani ya Legend ndani ya Simba nani alie ichafua hiyo thamani ni Simba wenyewe
Simba Wana wachezaji wengi walio ipambania Ile klabu kwa jasho lao lote wakati wa mafanikio walivyokuja kuondoka heshima yao yote imefutwa sasa hivi ukimtaja Aish ndani ya Simba ni kama hamna kitu kwa jinsi walivyoichafua taswira yake
Angalia Mazingira ya Mohamed Hussein kuondoka kosa lake ni nini? Mohamed Hussein ameshindwana na Simba kimaslahi amepata sehemu yenye maslahi bora zaidi kama mchezaji angefanya nini
Mfano Yanga wameachana na Khalid Aucho misimu huu baada ya kushindwana kwenye masuala ya kimkataba umesikia sehemu yoyote Yanga wakichafua taswira ya Aucho".
Mchambuzi Nasri Khalfan akizungumza kupitia Sports Arena ya Wasafi FM.