Aliyewahi kuwa kiungo wa Singida Black Stars Bruno Gomez (Barosso) ametangaza kuacha mpira kwa muda kutokana na maumivu ya Enka na goti yanayomsumbua kwa muda mrefu sasa.
Bruno alianza kuumia Enka akiwa Tanzania na hata baada ya kuamua kurudi nyumbani Brazil aliendelee kucheza kwa kujilazimisha lakini kwa sasa imeshindikana kuendelea!
“Kwa sasa sina timu, sina wakala wala mtu yoyote wa kunihudumia isipokuwa mimi, juhudi zangu na Imani yangu..!” - Sehemu ya Maneno ya kiungo huyo Raia wa Brazil.