TIMU ya Madagascar imefanikiwa kutinga Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Madagascar katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana limefungwa na winga wa Saint-Denis FC, Toky Niaina Rakotondraibe dakika ya 116.
Madagascar sasa itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya mabingwa watetezi, Senegal na Morocco zinazomenyana usiku huu Uwanja wa Mandela Jijini Kampala, Uganda.
Fainali ya CHAN 2024 itapigwa Agosti 30 Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi nchini Kenya ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Agosti 29 Uwanja wa Mandela, Kampala.