Shirikisho la soka la Sudan, limempatia kocha wa timu ya Taifa ya Sudan, Kwesi Appiah, Cheki ambayo haijajazwa kiwango cha pesa ili aandike kiasi chochote cha pesa anachokihitaji.
Timu ya taifa ya Sudan imekuwa na mafanikio makubwa chini ya Kocha huyo raia wa Ghana,
Tangu Appiah apewe timu mwaka 2023 amefanya badiliko makubwa sana katika kikosi hicho, ameifanya timu hiyo kuwa hatari, imara na kucheza mpira unaovutia
November 2024 alikiongoza kikosi hicho kufuzu michano ya AFCON 2025 lakini pia kocha huyo amekiongoza kikosi hicho kuiondosha timu ya taifa ya Nigeria kwenye michuano ya CHAN kwa kuwafunga magoli 4-0