TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji, Polisi FC kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa michuano ya ‘Better APR FC Pre Season Tournament’ leo Uwanja wa Pele, Nyamirambo, Kigali nchini Rwanda.
Polisi FC ilianza kupata bao kupitia kwa kiungo Mnyarwanda Alain Kwitonda dakika ya 21, kabla ya kiungo mwingine Mtanzania, Tepsi Evance Theonasy Prosper kuisawazishia Azam FC dakika ya 36.
Na kwenye mikwaju ya penalti kipa Zuberi Foba aliibuka shujaa kwa kuokoa penalti za Polisi FC.