Series inayofanya vizuri kwasasa kwenye mitandao ya kijamii hasa YouTube, Dunia, inaendelea kujizolea mashabiki lukuki na sasa imeingia kwenye tafrani kwa watazamaji wake.
Kelele zinazozusha hisia ni kwamba msanii Matilda ambaye amekuwa akikubalika kwenye pati yake akicheza kama mke wa nje wa Manyanya na kumfanya Vaileth kukosa raha.
Matilda au Matty amejizolea umaarufu mkubwa kiasi kwamba amekuwa hata akikosekana washabiki wake wanalia, Matty kwasasa hayupo kwenye series hiyo na amepachikwa mdada mwingine akiigiza kama Matty.
Malalamiko ni mengi wadau wakimkataa wakidai hafanani na Matty, ingawa yeye mwenyewe anawaomba mashabiki wa Matty orijino wamvumilie na atakaa sawa sawa.
Mambo Uwanjani Blog hivi karibuni itamleta kwenu msanii huyo na kuwajulisha ametokea wapi na yupo wapi Matty orijino ingawa ukweli ni kwamba mchumba wake amekataa kuendelea na series hiyo ya Dunia.