Wachezaji wawili wa zamani wa Yanga SC, Djuma Shabani na Chico Ushindi, wamejiunga na klabu maarufu ya AS Vita ya nchini Congo DRC, hatua inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Afrika.
Djuma Shabani - Beki wa Kulia Maarufu
Beki wa kulia Djuma Shabani, ambaye aliwika kwa kiwango cha juu akiwa na Yanga SC, amethibitishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa AS Vita. Djuma alikuwemo katika orodha ya wachezaji muhimu wa Yanga SC, akionyesha uwezo mkubwa na ufanisi wa kipekee kwenye safu ya ulinzi. Akiwa na Yanga SC, aliisaidia timu kuwa na ulinzi thabiti, na sasa anarejea AS Vita, ambako alionyesha ubora wake kabla ya kuhamia Yanga. Djuma, ambaye aliichezea AS Vita kwa mafanikio makubwa, amerudi kuungana na wachezaji wenzake.
Chico Ushindi - Winga
Kwa upande mwingine, winga maarufu Chico Ushindi, ambaye pia aliwahi kuichezea TP Mazembe, amejiunga na AS Vita. Chico mwenye uwezo wakupiga mipira ya hatari. Uhamisho huu unaleta mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji ya AS Vita, ambapo wapenzi wa soka wanatarajia kuona michango ya kibinafsi kutoka kwa mchezaji huyu ambaye ana uzoefu mkubwa
