Beki wa kushoto wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Hussein (28) anamaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi mwishoni mwa msimu huu na taarifa za kuaminika ni kuwa Mohamed Hussein ameipa kipaumbele zaidi Simba SC katika mkataba mpya kabla ya kuanza mazungumzo na klabu zingine
- Pia Klabu ya Kaizer Chiefs inahitaji kupata saini ya Mohamed Hussein katika dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu ujao na mchakato wa kumsajili beki huyo kutoka Simba SC utaanza baada ya Ligi ya PSL kumalizika.
