KAMPUNI maarufu ya michezo ya kubashiri, betPawa, imesaini mkataba wa mwaka mmoja a wenye thamani ya Sh 639,466,554 kwa Ligi ya Mpira wa Kikapu (BDL) ya mkoa wa Dar es Salaam.
Huu ni udhamini wa kwanza na wa kihistoria katika mpira wa kikapu hapa nchini usainiwa jana ambapo mkuu wa Maendeleo ya Michezo na CSR wa betPawa Raquel Puig pamoja na Katibu mkuu wa BD, Mpoki Mwakipake katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Don Bosco, Upanga jana.
Akizungumza katika hafla hiyo, Puig alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kuchangua maendeleo ya michezo nchini, hasa mpira wa kikapu ambao ni moja ya michezo pendwa duniani





