KOCHA Bakari Nyundo Shime ameita wachezaji 30 kuunda kikosi cha awali cha timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wanawake (WAFCONN 2025) ambacho kitaanza na michezo ya kirafiki katika Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hao ni pamoja na makipa; Naijat Abbas (JKT Queens), Asha Mrisho (Mashujaa Queens) na Janet Shija (Simba Queens).
Mabeki ni; Fatuma Issa (Simba Queens), Vaileth Nicholaus (Simba Queens), Lidya Maximillian (JKT Queens), Juletha Singano (Juarez, Mexico), Esther Maseke (Bunda Queens), Anastazia Katunzi (JKT Queens), Noela Luhala (ASA Tel Aviv University, Israel) na Christer Bahera (JKT Queens).
Viungo ni; Enekia Kasonga (Mazatlan FC, Mexico), Donisia Minja (JKT Queens), Asha Ramadhan (Yanga Princess), Maimuna Kaimu (ZED FC, Misri), Janeth Christopher (JKT Queens), Suzan Adam (Tutankhamun, Misri), Agnes Palangyo (Yanga Princess), Elizabeth Chenge (JKT Queens) na Aisha Mnunka (Simba Queens).
Wengine ni Stumai Abdallah (JKT Queens), Aisha Masaka (Brighton & Hove Albion, England), Clara Luvanga (Al Nassr, Saudi Arabia), Winfrida Gerald (JKT Queens), Hasnath Ubamba (FC Masar, Misri) na Diana Lucas(Trabzonsper, Uturuki) na Mary Siyame (Fountain Gate Princess), wakati washambuliaji ni Opa Clement (Juarez, Mexico) na Jamila Rajab (JKT Queens).
Kocha Bakari Nyundo ameiambia Bin Zubeiry Sports - Online kwamba watakuwa na michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mei 30 na Juni 2 Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Morocco kwenye Fainali za WAFCON zinazotarajiwa kuanza Julai 5 hadi 26.
Twiga Stars imepangwa Kundi C pamoja na mabingwa watetezi, Afrika Kusini ‘Banyana Banyana’, Ghana ‘Black Queens’na Mali ‘The Female Eagles’, wakati Kundi A kuna wenyeji, Morocco, Zambia, Senegal na DRC na Kundi B linazikutanisha Nigeria, Tunisia, Algeria na Botswana.
Hii ni mara ya pili tu Tanzania inashiriki WAFCON Afrika baada ya 2010 ilipokuwa chini ya Kocha mwingine mzalendo, Charles Boniface Mkwasa..

