Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa kesho atawakosa nyota wake muhimu ikiwemo Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda na Aziz Ki watakapoikabili Fountain Gate Ugenini.
"Ni kweli tuna baadhi ya wachezaji majeruhi kama Aucho, Pacome bado hajawa tayari, Musonda anahisi maumivu kidogo si makubwa lakini hatuwezi kumuhatarisha pamoja na Azizi Ki ana maumivu ya muda mrefu."
"Nawaheshimu wachezaji wote. Mimi si kocha wa kulalamika kwamba sina huyu au yule hapana nitampa nafasi kila mchezaji. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo itatuwezesha kufika mwezi Mei tukiwa imara.Kwa sababu kila mchezaji atakuwa amepewa muda wa kucheza. Hilo ni jambo muhimu sana kwangu."
Miloud Hamdi, kocha mkuu wa klabu ya Yanga Sc
