Beki wa Kati wa timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya JKT Tanzania, Wilson Nangu ataendelea kusalia kwenye Klabu yake ya sasa ya JKT Tanzania akihudumu kwenye Mkataba wake alionao na Waajiri hao.
.
Beki huyo ambaye anasifika kwa matumizi makubwa ya akili na nguvu kiasi ameiambia FUTBAL PLANET kuwa kwa sasa akili yake ni kuipambania nembo ya Klabu yake ili iweze kumaliza nafasi za juu lakini ameweka wazi kuwa yupo tayari kwenda sehemu nyingine kutafuta changamoto endapo kutakuwa na timu itakayofika dau ambalo JKT Tanzania watakuwa wanalihitaji.
.
"Mimi kiukweli malengo yangu na Klabu yangu ya JKT Tanzania nataman timu imalize kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi pia bado nina Mkataba na JKT Tanzania kwahiyo nipo sana kwenye timu hii na kama kuna timu inanihitaji basi wakae mezani baa waongee na uongozi wa timu yangu"
Amesema Wilson Nangu beki wa wa JKT Tanzania
