Timu ya Singida Black Stars imetupwa nje kwenye michuano ya kombe la Muungano baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 6-5na timu ya JKU katika uwanja wa Gombani, Pemba.
Timu hizo zimefikia hatua hiyo baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya mabao 2-2, Victorian Adebayor alitangulia kwa bao lake alilofunga dakika ya 6 lakini wakaongeza la pili kupitia Iddi Khalid Gego dakika ya 25.
JKU walipata bao lao la kwanza kupitia Tariq Mohamed dakika ya 28 na Freddy Seleman dakika ya 45, sasa Singida Black Stars wataisubiri Simba SC katika mchezo wao ufuatao wa Ligi Kuu bara
