SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Dk. Samia Samia Suluhu Hassan imegharamia usafiri na malazi kwa klabu ya Simba kwenye mchezo wake wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Stellenbosch Jumapili.
Katika barua yake ya shukrani kwa Rais Samia, Rais wa Simba SC, Mohamed 'Mo' Dewji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi amesema;
"Tumepokea kwa moyo wa shukrani mchango wa malazi na usafiri kuelekea mchezo wetu wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaofanyika Afrika Kusini,".
