Mchambuzi maarufu wa kituo cha redio ya UFM, Salama Ngale amesema kwamba wapinzani wa Simba, Stellenbosch si lolote na si chochote na Simba ijiandae kucheza fainali kwani hawana uwezo wa kuwazuia.
Nimefuatilia clips za wapinzani wa simba nusu fainali shirikisho Stellenbosch ya Afrika Kusini niseme tu hawa sio tishio, ni timu ya kawaida kabisa, simba waweke mipango ya fainali. Stellenbosch ni timu inayocheza mpira wa kawaida kabisa
Kilichowaponza Zamalek ni kushindwa kuvuna udhaifu wa Stellenbosch na kuwaruhusu kupata nafasi 1 ambayo wameitumia vizuri na kufuzu nusu fainali, pia uchezaji wa zamalek katika mashindano haya haukuwa wa viwango vya kikubwa kama tuonavyo kwa Waarabu wengine kama Mc Alger na Al Ahly
Hawa Stellenbosch uwezo wao uwanjani hautofautiani kabisa na Singida BSS au Tabora United, simba wana kila sababu kuipopoa timu hii ya chocolate home and away. Huu ni uchochoro kwa simba, hawa jamaa ni weupe kabisa hawako aggressive
Wana uchezaji wa kawaida kabisa hawa, simba inapaswa kuendeleza pira biriani la kasi na kufosi magoli, chemistry ya Simba ni ya kikubwa sana kulinganisha na wahun hawa wa bondeni alafu wengi ni vijeba wazito hawana kasi kama ile ya Orlando Pirates au Mamelod Sundowns
