Timu ya Mamelodi Sundown's ya Afrika Kusini imeendeleza ubabe wake wa kutokubali kufungwa na Al Ahly baada ya kuibana mbavu na kutoka sare tasa 0-0.
Miamba hiyo iliumana jioni ya leo mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, mchezo mwingine ni kati ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Pyramids ya Misri.
