Mtuma salamu wa muda mrefu katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini Joseph Mwita maarufu General Mwita Kiyalo amefariki dunia.
Kwa mujibu wa Nassoro Yusuph ambaye pia ni mtuma salamu mkongwe ameiambia Mambo Uwanjani Blog kuwa Mwita amefariki katika hospitali ya Muhimbili na msiba upo Tabata Chang' ombe jijini Dar es Salaam.
Yusuph amedai katika uhai wake Mwita alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Figo ambalo limeondoa uhai wake, mbali ya kuwa mtuma salamu, ni shabiki wa kutupwa wa Yanga.
