ALIYEWAHI kuwa mpenzi wa nyota wa bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna ametoa ujumbe mzito akiwataka wanawake wenzake waliopo katika uhusiano na wanaume wasiojielewa, wasio na malengo na wanaonyanyasa wanawake wajiondoe haraka.
-
Mwimbaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja amesisitiza kwamba wanaume hawafanani wapo wenye moyo mzuri na wapo waovu na wakorofi waliojaa sumu ingawa kutambua nani ni nani ndiyo shida.
-
Tanasha amesema kabla ya kuingia katika uhusiano wanawake wanatakiwa kutofautisha tabia za wanaume wa kweli na makanjanja wa mapenzi na pia wajue kutofautisha kati ya upendo wa kweli na uhusiano usiofaa kwa ustawi wao na vizazi vijavyo.
-
"Ninataka kuzungumza na wanawake kwa sababu mara nyingi tunabeba mzigo wa mahusiano yenye sumu," Tanasha amesema. “Tunahitaji kuwafundisha binti zetu, dada na ndugu zetu kuhusu wanaume hao,” akahimiza.

