Msemaji wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe ametangaza kuacha kazi iwapo wataji zao Simba wakiweka hadharani lisiti ya malipo na jumla ya mchango waliokusanya wa kulipa deni lao la CAF kupitia kampeni ya "Tunawajibika pamoja"
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagema, Kamwe amesema "Hili sitanii. Kuna Jasho la wengi limepigwa wakiaminishwa kuwa ni KUWAJIBIKA. Tukilikalia hili kimya, huu Utapeli utashika kasi.
"Sitaki ngonjera, watoe karatasi moja ya tu ya Ushahidi kuwa Ule mchango kweli Walilipa Lile deni. Kesho asubuhi Naacha Kazi".
Utakumbuka Simba walianzisha kampeni ya "Tuwajibika Pamoja" kwa lengo la kuchangia fedha za kulipia faini iliyotokana na makosa ya mashabiki wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchango huo ulianza rasmi Januari 15, 2025 na mara ya mwisho Simba kutoa taarifa ya kiasi cha pesa walizokunyasa ilikuwa Januari 21, 2025 ambapo walikuwa tayari wamekusanya Tsh 64,270,584/=
