Yanga kumlipia deni Gamondi
Wakati maswali yakiibuka juu ya kifungo cha mechi tatu cha aliyekuwa kocha wa Yanga, Miguel Gamondi pamoja na faini, TPLB imesema Yanga ndiyo itakayomlipia faini.
Gamondi amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini Sh2 milioni kwa kosa la kumsukuma na kumuangusha kocha wa viungo wa Singida Black Stars, Sliman Marloene baada ya majibishano yaliyotokea wakati timu hizo zikienda mapumziko katika mchezo uliopigwa Zanzibar
Akizungumza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema adhabu ya kulipa fedha aliyopewa Gamondi na Bodi hiyo italipwa kama ilivyotakiwa.
.
“Mhusika ndiye anayesimamia adhabu yake kwa sababu inamhusu yeye. Kuhusu namna ya kulipwa sisi tunatakiwa kuikata Yanga na wao ndio watamalizana kama wanamlipia au watamdai."