Tukifungwa na Azam tutauza ice cream Buguruni- Abbas
Na Ikram Khamees
Afisa Habari wa Coastal Union ya Tanga amesema endapo timu yao itafungwa na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu bara Jumapili ijayo basi wachezaji wake wataamua kufanya kazi ya kuuza ice cream kuanzia Buguruni Tazara kilipo kiwanda cha Azam mpaka Kariakoo.
Akizungumza leo katika kipindi cha Sports Arena kinachorushwa na Wasafi FM, msemaji huyo amedai uongozi wa Coastal Union umekutana na wachezaji na benchi la ufundi na kumaliza tatizo lililokuwepo.
"Kwasasa timu yetu ipo vizuri na tumeshamaliza tatizo hivyo timu itakayokatiza mbele yetu itakutana na kichapo, Azam FC tutakutana nayo Jumapili tutegemee kupata ushindi" alisema.
Coastal Union imetokea kufanya vibaya kiasi kwamba ikamfukuza kocha wake David Ouma raia wa Kenya, hata hivyo licha ya kumfukuza Ouma, iliendelea kufanya vibaya wmbapo imepoteza mechi mbili mfululizo na ikitoka sare moja