Tuko nyuma ya 2-0 kwa Al Ahli Tripoli- Ahmed Ally

Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kimuonekano Simba SC ni kama imefungwa mabao 2-0 kwa sababu wapinzani wao waliwazidi kwenye maeneo mawili.

"Mpaka sasa tupo nyuma goli 2-0 dhidi ya mashabiki wa Al Ahli Tripoli. Goli la kwanza kuujaza uwanja wao wote kwa mashabiki 50,065.

Hili kwetu ni deni na sisi kuujaza. Sina hofu na hilo kujaza uwanja wa Mkapa. Wao walijaa na sisi tunapaswa kujaa. Goli la pili mashabiki wote kuvaa jezi za timu yao, na hilo tuna wajibu wa kwenda kusawazisha. Kila Mwanasimba atakayekuja uwanjani anatakiwa kuvaa jezi mpya ya msimu hii.”

“Kwa kutambua kwamba tunapaswa kuvaa jezi za aina moja, mdhamini wetu wa jezi amepunguza bei kwa punguzo maalumu. Jezi zitauzwa Tsh. 30,000 na zinapatikana kwenye maduka ya Sandaland The Only One lakini pia kwa atakayekuja uwanjani na kununua jezi yake ya Tsh. 30,000 atampa zawadi ya tiketi ya mchezo bure.”

“Tunapohimiza watu wavae jezi, tunahimiza watu wavae jezi orijino. Tuseme wazi kwamba tayari tuna taarifa ya mzigo wa jezi feki kuingia nchini. Mdhibiti wa kwanza wa jezi feki ni wewe Mwanasimba, usikubali kununua jezi ya aina hiyo.”

“Ili kupendezesha uwanja. Wanaume wote siku ya Jumapili tutavaa jezi nyekundu, wanawake wote watavaa jezi nyeupe na watoto wote wa Simba watavaa blue.

Kama huna jezi nyekundu na wewe ni mwanaume kanunue jezi mpya na kama wewe ni mwanamke huna jezi nyeupe kanunue jezi mpya kwa bei ya punguzo.”- Ahmed Ally.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI