Simba itashinda dhidi ya Al Ahli Tripoli

Mchambuzi wa michezo kutoka radio Crown FM, Jemedari Said amesema Simba SC itashinda dhidi ya Al Ahli Tripoli kwakuwa timu hiyo si nzuri ingawa pia sio mbaya kivile.

“Al Ahly Tripoli sio timu nyepesi na sio timu ngumu. Watu wanapaswa kujua Simba SC ni kigogo wa Afrika. Mimi nitashangaa Simba SC wakifungwa na hii timu. Hayo mambo ya Mabilioni siyapi nafasi. 

National Al Ahly ya Misri waliwahi kuja nchini na Ramadhan Sobhi aliyetoka West Brom na walimsajili kwa Mabiliono ya fedha, lakini walipoteza dhidi ya Mnyama"
.
"Simba ni mkubwa kwa hiyo timu ya Libya. Tripoli kafungwa hadi na Biashara United ya Mara, timu hii ndiyo ije kuifunga Simba SC? 

Unadhani Simba SC kwanini hawajaanza huko uchochoroni kama walivyoanza wengine? Sio kwa bahati mbaya. Hawajapata sifa hii kwa uongo, wamejijenga “
.
—JEMEDARI SAID,Mchambuzi CROWN FM.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI