Mpya, Yusuph Kagoma alisaini miaka mitatu Yanga

“Tulianzisha maongezi ya muda mrefu na Singida Fountain Gate ilikusudi Yanga imnunue rasmi Yusuf Kagoma. Masharti waliyotupa Singida ni kulipa million 30 na sisi tulisema tutalipa kwa awamu mbili na tarehe 30 mwezi wa nne tuliilipa Singida Fountain Gate .
Baada ya kufanya malipo klabu ya Yanga iliruhusiwa kufanya mazungumzo na Mchezaji kwaajili ya maslahi binafsi na baada ya hapo klabu ya Yanga ilimtumia Yusuph kagoma tiketi ya ndege ili aje kusaini Mkataba na hivyo Kagoma aliwakilishwa na Wakili wake Bwana Léonard na yeye mwenyewe akaweka saini. Kwahiyo tunaweza kusema Kagoma bado ni mchezaji wetu"

"Mpaka sasa tunaongea Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc tulimsaini miaka mitatu na tukamtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 - 2025" - Simon Patrick, Mkurugenzi wa Sheria wa Young Africans SC.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI