Mashujaa FC yaichabanga Coastal Union

Timu ya Mashujaa FC ya Kigoma jioni ya leo imeendeleza ushindi baada ya kuilaza Coastal Union bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa KMC Complex uliopo jijini Dar es Salaam.

Hali si nzuri kwa Coastal Union ambao wametoka kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, huku mambo yakiwa mazuri kwa Mashujaa FC ambao wakipata ushindi wake wa pili.

Crispin Ngushi akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, amekuwa na msimu mzuri, aliifungia Mashujaa bao la ushindi dakika 14 likiwa ni bao lake la pili tangu kuanza msimu huu


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI