Kaduguda adai Ateba anafaa kucheza beki na si mshambuliaji

Aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa klabu ya Simba SC Mhina Mohamed Kaduguda amemtazama vema mshambuliaji wa Simba Leonel Ateba na kudai anafaa kucheza beki na si mshambuliaji.

Kaduguda ambaye pia ni kocha kitaaluma, aliwahi kuwakosoa washambuliaji wawili wa Simba Pah Omary Jobe na Freddie Michael kwamba si lolote na hata viwango vyao ni vidogo na akataka waachwe jambo ambalo limetimia.

"Beki kazi yake inajulikana,Kiungo kazi yake inajuliakana na mshambuliaji sifa yake inajulikana. Striker hawezi kuwa na goli 1 na Assist 8, kwa assists hizo alipaswa kuwa na magoli angalau manne, kwanini uwe na Assists nyingi kuliko magoli na wewe ni striker", alisema Kaduguda

Mhina Mohamed Kaduguda


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI