Gamondi awataka wachezaji Yanga kuongeza juhudi

Kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi amewataka wachezaji wake kuongeza ubora kwani timu pinzani zimejipanga kupambana nao na kuibuka na ushindi na ipo siku mchezo utakuwa mgumu kwao.

"Kila timu sasa inataka kuifunga Yanga, inabidi tupambane, tusijidanganye kuwa tupo kwenye mstari salama, ninawaambia haya hata wachezaji wangu, wanatakiwa kila siku waongeze juhudi na mazoezi zaidi ili tuwe bora kila kukicha kwani Wenzetu nao wanaongeza ubora ili watufikie au watupite,

"Na si kwenye soka tu, hata kwenye maisha ni lazima uwe na presha ya kusaka maisha, kuweza kulipa kodi, kutunza nyumba, kulisha watoto, kuwalipia ada, yote hii ni presha na hiyo ndiyo inakufanya uwe makini na ujitume.” -Amesema Gamondi.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI