Azam FC yabanwa na Pamba Jiji

Timu ya Azam FC usiku wa leo imeendelea kuachia pointi baada ya kulazimishwa sare tasa 0-0 nyumbani mbele ya timu iliyopanda daraja ya Pamba Jiji FC ya Mwanza mchezo wa Ligi Kuu bara kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.

Kwa mwenendo huo hali inaonekana si nzuri hasa baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, na pia ikianzs vibaya kwenye ligi hiyo kwa kutoka sare tasa na JKT Tanzania.

Mpaka sasa Azam imefikisha pointi mbili huku wapinzani wao Simba wana pointi 6 wakiwa wamecheza mechi mbili kama wao,.Yanga nao wana pointi tatu wakiwa wamecheza mechi moja, mechi itakayofuata ni dhidi ya Simba.

Hata hivyo mwamuzi bora Tatu Malogo aliwanyima bao la wazi wazi Pamba Jiji

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI