Kikosi cha Azam FC kimeshaondoka kwenye viunga vya Azam Complex, kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa safari ya nchini Morocco kuweka kambi ya wiki mbili ya maandalizi ya msimu mpya 2024/25.
Azam FC itashiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, Ngao ya Jamii na Ligi Kuu bara hivyo maandalizi yao yatakuwa na umuhimu mkubwa na nchi ya Morocco wameona sehemu sahihi kwao