Agosti 3 Simba kumtambulisha Mpanzu

Na Salum Fikiri Jr

Klabu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi Agosti 3 mwaka huu wakati wa tamasha lake la Simba Day inatarajia kumtambulisha winga Elie Mpanzu toka DR Congo kama mchezaji wake mpya.

Simba itamkata Willy Onana  baada ya kocha wa Wekundu hao kumkataaa mazima na hivyo mabosi wa timu hiyo wamelazimika kumfuatilia Mpanzu na kuongeza dau analolitaka.

Simba ilishaachana na Mpanzu na kuamua kumtumia tiketi ya ndege Onana na kusafiri kuwafuata wenzake waliotangulia Misri, lakini jana Simbaisha kocha wa timu hiyo amemkataa waziwazi Onana na kutaka aletwe fasta mbadala wake ama sivyo timu itayumba kwenye Ligi na michuano ya kimataifa.

Jumamosi hii, kama mambo yakienda sawa atatambulishwa kwenye Simba Day, kama wakimpata Mpanzu watakwenda kugombea msimu ujao; Wakongomani wameniambia Mpanzu ni namba 10 ambaye muda mwingine anacheza kama winga kilisema chanzo changu


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI