Mke wa Profesa Jay afunguka makubwa

Mke wake na Joseph Haule au Professor Jay wakati akiwa kwenye Interview na chombo kimoja cha TV amefunguka namna ambavyo walivyoweza kukutana na mume wake professor Jay kabla hawajawa wapenzi

Ambapo kwa maelezo yake amesema kuwa yeye na Professor Jay walikutana American chips ya kinondoni ambapo alikuwa anaelekea field hivyo wakati huo ilikuwa asubuh alisimamishwa na baadae akaombwa namba ila alivyomuuliza jina akaambiwa anaitwa Joseph

Lakini kuhusu kumpa namba alimpatia kwasababu wakati joseph anasimamishwa aliongeleshwa kwa heshima pia mbali na hivyo hakuwa anafahamu kama ni star mkubwa na maarufu lakini alikuwa anafikiri ni mpita kwasababu alikuwa si mpenzi wa mitandao