Azam FC imemtambulisha, Ever Meza, kama kiungo wao mpya aliyenunuliwa kutoka klabu ya Leonnes ya Colombia.
Meza, raia wa Colombia aliyezaliwa Julai 21, 2000; alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Alianza FC ya huko huko Colombia.
Amesaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka Azam Complex hadi mwaka 2028.
Karibu sana Ever William Meza Mercado