Kupitia post ya @trtafrikasw wameweka post ambayo wanasema Kwa mujibu wa Jariba la kutoa Takwimu za michezo duniani la Transfer Market.
Limetoa orodha ya vilabu 10 vyenye thamani zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki, na katika orodha hiyo Klabu ya Simba ya Tanzania ndio ghali zaidi ikionyeshwa kuwa thamani yake ni Euro milioni 3.25 sawa na Tsh bilioni 8.937.
Klabu ya Yanga inashika nafasi ya pili kwa kuwa na thamani ya Euro milioni 1.85 ambayo ni sawa na Tsh bilioni 5.085.
Katika orodha hiyo vilabu vitatu vya mwanzo vinayoka Tanzania lakini pia katika vilabu 10 vilabu 6 vinatoka Tanzania.
Vilabu vya Congo Dr vinaongozwa na TP Mazembe ambayo ipo nafasi ya nne.
Unakubaliana na orodha hiyo kwa asilimia ngapi?? Dondosha comment yako hapa chini.