Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AZAM FC YALAMBA MKATABA MNONO



Azam FC imeingia makubaliano ya ushirikiano na vituo vya kulea vipaji (academies) nane za mikoa mbalimbali nchini.

Vituo hivyo nane vitakuwa ni 'AZAM FC CENTERS', vikituwakilisha katika mikoa husika, vikiwa na jukumu la kutafuta vipaji vya wachezaji vijana wa Kitanzania, watakaokuja kujiunga na kituo chetu 'Azam FC Academy' kutokana na mahitaji ya timu yetu.

Baadhi ya vituo hivyo tulivyoanza navyo ni JK7Pro Football Center (Tanga), Tutes Hub Sports Center (Songea), Maendeleo Youth Sports Center (Mtwara), Kilwa Youth Sports Center (Lindi).

Vingine ni Muleba Youth Sports Center (Kagera), Mwanga City Sports Center (Kigoma), Rungwe Youth Sports Center (Mbeya) na Korogwe Youth Soccer Center (Korogwe).

Azam FC tutavipa kipaumbele vituo hivyo katika kuvuna vipaji vya vijana, pale tutakapokuwa na uhitaji wa wachezaji kwenye kituo chetu.

Lakini sisi kama Azam FC tunaothamini vipaji vya vijana wadogo, tutaendelea na jukumu letu la kila mara la kuvuna vipaji popote pale nchini, tukiendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini.

Tayari makubaliano kati ya vituo vyote hivyo na Azam FC yameingiwa kwa mikataba rasmi, zoezi lililosimamiwa kwa ukaribu na Vice Chairman, Omary Kuwe.

Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, hivi karibuni benchi letu la timu za vijana, litatembelea vituo hivyo (Azam FC Centers) kwa ajili ya kukutana na makocha wanaofundisha vijana hao, lengo likiwa ni kuwajenga zaidi na kuwapa vigezo vya aina ya wachezaji wanaowahitaji.

Kwa kuanzia, tumeanza na vituo hivyo nane, lakini katika ramani yetu tumepanga kuifikia Tanzania nzima kwa kuwa na 'Azam Centers' katika mikoa yote nchini.

Tunaamini kuwa kupitia programu hii, klabu yetu itaweza kuvuna vipaji bora vya vijana wa Kitanzania na kuviendeleza zaidi pale watakapofika kwenye kituo chetu 'Azam FC Academy'.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...