Klabu ya Soka ya Polisi Tanzania, ‘imeichimba mkwara’ Yanga SC kuelekea mchezo wao wa kesho wa michuano ya AzamSportsFederationCup utakaopigwa saa 1:00 usiku katika dimba la Azam Complex, Chamazi.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Polisi wameweka andiko lao likitoa onyo kwa Yanga ya kwamba ni bora wangeomba mechi hiyo iahirishwe ili wajiandae na mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad hapo Jumamosi.
“Bora wangedeka tu, lakini kwa vile wamekubali wenyewe hawataamini macho yao. Katika kipindi kama hiki tutawatupa rumande mpaka Jumamosi bila dhamana na hatuogopi kutupiwa yale mavitu yao” inasema Polisi Tanzania FC.
