Chama cha Soka Misri (EFA) leo kimemtangaza Hossam Hassan mwenye umri wa miaka (57) kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo 'Mafarao', Hassan anachukua nafasi ya Mreno, Rui Vitoria ambaye ametimuliwa hivi karibuni kutokana na mwenendo usioridhisha kwenye fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoelekea kufikia tamati huko Ivory Coast.
Kocha huyo mpya wa Misri Hossam Hassan, aliwahi kuwa nyota wa timu ya taifa ya nchi hiyo akiichezea michezo 178 huku akifunga mabao 69, Hossam Hassan amefanikiwa kushinda mataji matatu ya AFCON akiwa na mafaro 1986, 1998 na 2006 Katika majukumu hayo ya kuinoa Misri, Hossam Hassan atasaidiwa na pacha wake, Ibrahim Hassan.
