Hatimaye timu ya taifa ya Mali usiku huu imeingia robo fainali ya michuano ya mataifa Afrika, AFCON nchini Ivory Coast baada ya kuilaza Burkina Faso mabao 2-1.
Kwa matokeo hayo sasa Mali imeingia robo fainali na inamngoja mshindi kati ya Morocco au Afrika Kusini watakaokutana saa 5 usiku.
Mabao ya Mali yamefungwa na Edmond Tapsoba dakika ya 3 na Lassine Sinayoko dakika ya 47 wakati la Burkina Faso limefungwa na Bertrand Traore, pia jana usiku Senegal ilivuliwa ubingwa na wenyeji Ivory Coast baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 9-8 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120