Mlinda mlango bora nchini kwa kipindi cha misimu miwili Djigui Diarra wa Yanga na Malia ameweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kutoka Ligi Kuu ya kuanza michezo 4 mfululizo katika michuano ya AFCON 2023.
Pia Diarra anaungana na walinda milango wengine Afrika ambao wamecheza mechi 4 mfululizo katika Afcon akiwemo Edouard Mendy wa Senegal,Llyod Kazapua wa Namibia,Stanley Nwabali wa Nigeria na Yahia Fofana wa Ivory Coast.