Taarifa za Uhakika zilizothibitishwa na mtandao huu ni kuhusu Victorien Adebayor kusain kunako Club ya Simba.
Ikumbukwe Adebayor alisajiliwa na Amazulu ambayo kwa Sasa inanolewa na Kocha wa Zamani wa Simba Pablo Franco , alisajiliwa msimu huu kuchukua nafasi ya Gabadinho Mhango.
Klabu ya Amazulu waliwasilisha malalamiko FIFA kuhusiana na mchezaji huyo kutoripoti kwenye kikosi kwa sababu zisizo na lakini Adebayor alishindwa Kulipoti kwasababu mipaka ya Niger ilifungwa Kipindi Taifa Hilo lilipofanya mapinduzi ya Kijeshi hivyo mipaka ilifungwa.
Adebayor hakufurahishwa na RS Berkane na pia hakupenda kujiunga na klabu ya Amazulu
Wakala wa winga na mfungaji bora wa muda wote wa Niger alikuwa Sokoni kutafuta Timu na inasemekana klabu ya Simba SC kupitia wakala wa Victorien Adebayor Ndiyo wamefanikisha mazungumzo kati Amazulu na Simba .
Hata Hivyo taarifa kutoka Kunako Club ya Amazulu Ni Kwamba wanamalizia Taratibu za kimkataba zinazomhusu Mchezaji, na dirisha dogo atatambulishwa kuwa Ni Mnyama