Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya African Football League au maarufu Super Cup, Simba SC leo wamezindua jezi mpya itakazotumia katika michuano hiyo inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Simba itacheza na timu ya Al Ahly ya Misri katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo imeamua kutoa jezi mpya ambapo mashabiki wake watalazimika kuzichangamkia kwa kununua kwa wingi.
Wadhamini wa jezi hizo Sandalend wameziweka hadharani jezi hizo ambazo zitatumika kwa ajili ya kucheza mechi za nyumbani na ugenini





