Klabu ya Yanga imetangaza kukamilisha Usajili wa aliyekuwa Nahodha wa Klabu ya AS Maniema Union na wa Ligi Kuu ya DR Congo Msimu wa 2020/21,Maxi Mpiana Nzengeli kwa Mkataba wa Miaka miwili.
Maxi mwenye Umri wa Miaka 23 anamudu kucheza winga zote mbili na Kiungo Mshambuliaji huku akisifika kwa kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki kandanda na akiwa Mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa ya DR Congo ambapo alikuwepo kwenye kikosi cha CHAN Cha DRC akicheza Sambamba na Mika Miche wa Lupopo na Zemanga Sonze wa Mazembe