Mjue Gift Fred, beki mpya wa kati aliyechukua nafasi ya Mamadou Doumbia

Na Salum Fikiri Jr

MIAKA kadhaa iliyopita Yanga SC lilikuwa jina kubwa nchini Uganda hasa kwa sababu ilizoeleka mara kwa mara kwenda kucheza na timu za huko na pia kusajili wachezaji mbalimbali. 

Ikumbukwe mwaka 1993 na 1999 Yanga ilienda kushinda ubingwa wa Klabu biogwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame, Yanga iliweza kusajili nyota mbalimbali nchini Uganda kama Hamisi Kiiza "Diego" ambao walitokea kujipatia umaarufu mkubwa. 

Yanga ikapotea machoni mwa Uganda na likabaki jina tu ambalo linaendelea kusikika pande mbalimbali za Afrika na dunia, umaarufu wa Yanga unatokana na na uwezo wake uliouonyesha msimu uliopita ambapo iliweza kufika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, pia iliweza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu bara na mengineyo. 

Ingawa tayari ina mchezaji kutoka Uganda Khalid Aucho, ikitaka kujiimarisha zaidi ili kushindana ndani na nje ya nchi. Kikubwa wanachokiangalia Yanga ni kufika makundi Ligi ya mabingwa barani Afrika.

Baada ya msimu uliopita kumsajili beki wa kati Mamadou Doumbia raia wa Mali, bado Yanga haijafanikiwa kwani mchezaji huyo alishindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Doumbia alisajiliwa kwa lengo la kusimama katikati akicheza na Bakari Mwamnyeto au Dickson Job, kushindwa kwake Doumbia kulimfanya kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia kumtumia Ibrahim Baka kama sentahafu. 

Baada ya kumalizika msimu wa 2022/2023 huku Yanga ikishinda mataji yote matatu, ikiwemo kombe la Azam Sports Federation Cup, ASFC au kombe la FA. 

Na pia ilianza na kubeba Ngao ya Jamii mwanzoni mwa msimu, dirisha kubwa la usajili limefunguliwa na Yanga ikaamua kuanza na beki wa kimataifa kutoka nchini Uganda. 

Sio siri mabingwa hao wa Tanzania bara walianza kumfuatilia kwa kina Gift Fred anayeichezea timu ya SC Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda, pia timu ya taifa, The Cranes. 

Gift ni beki wa kati anayecheza namba 5 au 4 na ana uwezo mkubwa wa kunyang' anya mipira, Gift ana ball control ni beki wa kisasa anajua kupiga pasi, anapiga chenga za maudhi anapanda mbele na kufunga.

Gift anaokoa kwa kuruka vichwa anacheza takolini, ana nguvu na anajua kukaba, kwa kifupi Yanga imepata beki mpambanaji na ndio maana The Cranes wamemfanya awe nahodha msaidizi. 

Beki huyo alionekana kwa mara ya kwanza dhidi ya Kaizer Chief katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga ilishinda bao 1-0. 

Mchezo huo ulikuwa wa maadhimisho ya Wiki ya Wananchi, Gift alizaliwa 1998  



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI