Mchezaji wa PSG, Kylian Mbappe ametua nchini Cameroon na kupokelewa na maelefu ya mashabiki huku ulinzi mkali ukiimarishwa dhidi yake.
Mbappe yupo Cameroon kwaajili ya kumtembelea baba yake kijijini pamoja na kuangalia miradi yake ya kusaidia jamii (hisani).
Mashabiki wengi wamejitokeza kumlaki staa huyo wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kuwasili kwenye taifa hilo la Afrika.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 24, atatembelea shule mbili za Yaounde na Douala ambazo zinafadhiliwa na taasisi yake ya hisani.
Mbappe atakuwa Cameroon kwa siku tatu ambapo kesho siku ya Jumamosi atakwenda Djebale ambapo ndipo kijijini kwa Baba yake Mzee Wilfried Mbappe raia wa nchi hiyo kabla ya kukimbilia ughaibuni Ufaransa na kuwa mwalimu