Taarifa zilizotufikia zinasema kwamba huenda duka kubwa la kuuza mavazi ikiwemo vifaa vya michezo la Sandaland muda wowote linaweza kuchukua nafasi ya Vunjabei na kuwa wadhamini wa jezi wa klabu ya Simba SC.
Sandaland ndiye atakuwa mzalishaji mpya na msambazaji wa jezi za Simba msimu ujao na tayari alikuwa China akifyatua uzi wa mnyama.