Aliyekuwa kocha Msaidizi wa Kocha wa Roberto Oliveira "Robertinho" wakifanya kazi pamoja ndani ya Klabu ya Vipers SC ya Uganda, Marcelo Cardoso Anatarajia kutua Nchini Kuungana na kikosi cha Simba SC na Kuwa Kocha Mpya Msaidizi kuchukua nafasi ya Kocha Juma Mgunda atakae ondoka Klabuni hapo Ifikapo mwishoni mwa msimu huu.
Cardoso raia wa Brazil atakuwa Kocha Msaidizi Namba moja Anatarajia Kuungana na Kocha Msaidizi namba mbili Ouanane Sellami raia wa Tunisia huku pia Klabu hiyo ikiwa Katika hatua za mwisho kumalizana na Kocha wa zamani wa Viungo Mtunisia Adel Zrane, Kuchukuwa nafasi ya Kelvin Mandla kuunda Benchi Jipya la Ufundi Klabuni hapo msimu Ujao 2023/2024.
