Mayele anawania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa CAF

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga SC Fiston Mayele ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi April wa Afrika ambapo anashindanishwa na mastaa mbalimbali wanaocheza barani.

Orodha hiyo imetolewa na mtandao wa @foot_africa mpaka sasa Mayele anashika nafasi ya pili kwa wachezaji waliopogiwa kura nyingi na zoezi bado linaendelea kwenye website ya Foot-Africa.com na zoezi bado halijafungwa mpaka sasa.

Msimamo hupo hivi

βš½πŸ‡¨πŸ‡² Vincent Aboubakar: (27%)
βš½πŸ‡¨πŸ‡© Fiston Mayele: (22%)
βš½πŸ‡©πŸ‡Ώ Riyad Mahrez: (18%)
βš½πŸ‡ΈπŸ‡³ Iliman Ndiaye: (14%)
⚽πŸ‡ͺπŸ‡¬ Mohamed Salah: (9%)
βš½πŸ‡²πŸ‡¦ Youssef En Nesyri: (7%)