Kocha Monastir aitabiria Yanga kufika nusu fainali

Na Shafih Matuwa

Kocha wa klabu ya US Monastir amesema Yanga ina mambo (2) mazuri yanayowabeba na wananafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali iwapo watayaongezea nguvu.

"Ubora wa kwanza wa Yanga wanaoongoza kundi letu ni uwepo wa kocha Nasreddine Nabi ambaye ameiweka Yanga mahali salama kimbinu na kwamba hata ukiwa mbele unaongoza kwa bao (1) unahitaji ubora kulilinda bao lako kwa kuwa Nabi ni kocha anayebadilika badilika"

"Tulipocheza na Yanga tukashinda (2-0) lakini muda wote hatukuwa na utulivu wa kuona kama tumemaliza mechi. Nawaheshimu sana (Yanga) kwa kuwa wanaonesha kuna kazi kubwa kocha wao amefanya.. Hata nilipokuwa nawafuatilia na kuangalia mechi zao sikuona kama kuna mchezo wamezidiwa umiliki wa mpira"

"Napenda wanavyocheza, wanakulazimisha, wakati wote wanataka mpira uwe katika miliki yao. Tulipocheza nao kisha kucheza na Tp Mazembe tuliona tofauti kubwa ilitosha kuona kwamba Yanga watakuwa washindani wetu wakubwa katika kundi letu"

"Silaha ya pili ya Yanga ni wale washambuliaji wawili kwenye eneo la mbele, yule namba 9 (Mayele) ni hatari anajua sana kufunga lakini pia anakasi. Kuna yule jezi namba 25 (Musonda) ndio tatizo zaidi, unapokuwa na washambuliaji wa namna ile wanawalazimisha mabeki kupoteza nidhamu yao kutokana na kasi yao. Kitu kibaya zaidi wanacheza kwa ushirikiano mkubwa"

"Kwangu mimi nawaona (Yanga) watafika mbali kama watabahatika katika droo kutokukutana na timu ngumu. Najiandaa kuwaona wanacheza nusu fainali "Darko Novic


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI