Rasmi, Tarimba awatuliza Yondani, Kessy, Yanga

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati maalumu ya mpito ya klabu ya Yanga , Abbas Tarimba amefanikiwa katika Juhudi zake za kumzuia beki Kelvin Yondani asisajiliwe na klabu ya Simba  mara baada ya kufikia makubaliano kwa beki huyo kuendelea kuitumikia klabu hiyo .

Jana tena Tarimba alifanya mazungumzo na Kelvin Yondani na mchezaji huyo kukubali Kuongeza kandarasi mpya klabuni hapo .

Inasemekana klabu ya Simba SC ilikuwa inamuwinda kwa hudi na Uvumba beki huyo lakini Jitihada zao zilishindwa kutokana na makubaliano kutofikiwa baina ya Simba SC na Kelvin Yondani .

Tarimba ambaye amesisitiza anataka kujiondoa katika kamati maalumu ya mpito ya klabu ya Yanga pia amefikia makubaliano na Hassan Kessy ili aweze kubaki klabuni hapo .